MJUMBE WA AU APORWA NCHINI AFRIKA KUSINI
Mjumbe huyo kwa jina la Gabriel Gundo, alikumbwa na mkasa huo alipokuwa akisafiri kutoka uwanja wa ndege wa OR Tambo kuelekea Sandton ili kuhudhuria mkutano wa AU.
Gundo mwenye umri wa miaka 55, alisimamishwa na waporaji waliovalia mavazi ya polisi na kuporwa fedha dola 500 za Kimarekani alizokuwa amebeba pamoja na noti kadhaa za fedha za ndani ya nchi.
Msemaji wa idara ya polisi amearifu kwamba uchunguzi unaendelea kufanyika kuhusiana na tukio hilo.CHANZO TRT SWAHILI
Chapisha Maoni