King wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz.
Mwandishi wetu
Kwa mujibu wa chanzo kilichoambatana na Diamond katika ziara ya kimuziki
iitwayo ‘Nana Tour’ nchini humo, staa huyo ambaye kwa sasa ni mpenzi wa
mjasiamali maarufu, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ amekuwa
akiumizwa na penzi la Omotola kitambo sana lakini hakuwahi kuzungumza
katika vyombo vya habari.
Staa wa Nollywood nchini Nigeria, Omotola Jalade Ekeinde ‘Omotola’.
“Diamond ana maumbo yake flani hivi amazing ambayo huwa anayapenda, siku
nyingi sana kabla hata hajakutana na Zari, alikuwa akituambia watu wake
wa karibu kwamba miongoni mwa wanawake mastaa ambao anawatamani awaweke
kwenye himaya ya penzi lake ni Omotola.
“Alisema anampenda kwa kila kitu kuanzia ufanyaji kazi wake, umbo lake
na hata umaarufu mkubwa alionao ndani na nje ya Bara la Afrika,”
kilisema chanzo hicho.
Baada ya chanzo hicho kueleza habari hiyo, mapema wiki hii, mtandao wa
nigeriafilms.com ulithibitisha maneno hayo kwa kuposti habari
iliyobainisha Diamond anampenda Omotola sanjari na mastaa wengine wawili
wa Nigeria anaovutiwa nao kimapenzi.
Akiwa hewani alipokuwa akihojiwa na redio moja jijini Lagos, Diamond
aliweka bayana kuwa anateswa na penzi la mastaa watatu Nigeria, Omotola,
Tonto Dikeh na Genevieve Nnaji.
“Jamaa kitambo sana anateswa na penzi la Omotola sasa leo kaongeza na
wengine wawili na ninavyomjua hashindwi kufanya kweli ingawa nina
wasiwasi kwa Omotola na Tonto maana wana waume zao labda ajiweke kwa
Genevieve ambaye hajaolewa,” kilikazia chanzo chetu.Diamond hakupatikana
ili kusikia kauli yake juu ya ishu hiyo.
CREDIT;GLP
Chapisha Maoni