Kijana mmoja aliyejitambulisha kwa jina moja la Rogers (pichani) raia
wa Uganda amekiri kufanya ngono na wanafunzi 712 wa vyuo vikuu
mbalimbali nchini Tanzania na Uganda na kuwaambukiza virusi vya UKIMWI
kwa kipindi cha miaka mitatu.
Rogers amesema alipogundua ana maambukizi ya HIV mwaka 2012 aliamua
kulipiza kisasi kwa kuambukiza wasichana wengi kadri iwezekanavyo. Hadi
kufikia mwaka huu alikwisha ambukiza wasichana 712 wote wakiwa wanafunzi
wa vyuo vya elimu ya juu kutoka Tanzania na Uganda. Vyuo vya Tanzania
ambavyo Rogers anadai kutembea na wanafunzi wake ni CBE Dar, IFM,
USTAWI, UDSM na TIA. Pia amedai kuwa kati ya wasichana wote 712
aliotembea nao hakuna yeyote aliyemrudia mara mbili wala kutumia condom.
"Sikuhitaji kumrudia mtu mara mbili maana ni kupoteza muda.
Nilijitahidi kadri niwezavyo kuwapata wengi ili kutimiza azma yangu ya
kuambukiza mamia ya wanafunzi." alisema Rogers.
Chapisha Maoni