
Idadi
ya vifo vinavyotokana na joto kali nchini India vimepita zaidi watu
1,000 huku hali ya joto ikikaribia nyuzi joto 50 katika baadhi ya
maeneo.

Vingi
ya vifo vimetokea katika jimbo la kusini la Telangana pamoja na Andhra
Pradesh, ambapo watu 1,118 wamekufa tangu wiki iliyopita.

Ripoti
zinaeleza watu wengine 24 wamekufa kutokana na joto kali huko Bengali
Magharibi pamoja na Orissa. Hali ya joto hilo inatarajiwa kupungua
katika siku chache zijazo.



Chapisha Maoni