Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’
Musa mateja
Akizungumza na gazeti namba moja la mastaa Bongo, Ijumaa Wikienda,
wikiendi iliyopita, Jokate alisema alishangazwa na maneno hayo ambayo
hakustahili kuyatamka kwani kama ni ishu ya mtu kula makombo mbona hata
yeye ni makombo na bado anakula makombo?
Jokate Mwegelo ‘Kidoti’
“Sijapendezwa na kauli ya Diamond na namshangaa sana, sijajua nini
kimemkuta maana mimi sijamtaka wala hakuna ambapo niliwahi kumwambia
kuwa ninatoka au ninamtaka Kiba, zaidi ya maneno ya watu kwenye
mitandao ya kijamii.
“Hata kama hilo lipo, bado sioni maana ya neno makombo kwani hata yeye
ni makombo na anakula makombo kwa Zari (Zarinah Hassan) kwani nani
asiyejua?” alihoji Jokate akionekana kuchukizwa na kauli hiyo ya Diamond
na kuongeza:
“Yawezekana labda maana ya neno hilo hatulijui ndiyo maana tunalisema
bila kuliangalia kwa umbali zaidi, hivyo ninachoweza kukisema ni kwamba
mimi sijawahi kumtaka wala kumhitaji hivyo sioni kabisa sababu ya msingi
ya kusema hivyo labda kama alikuwa na maana nyingine tofauti na hiyo.”
Credit:GPL
Chapisha Maoni