KIONGOZI
wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Tanzania mwaka 2015/2016, Juma Khatib Chum,
akimkabidhi chandarua mtoto Fatmat Abdalla Mohammed, anayeishi na VVU
mara baada ya kuonyesha hali halisi ya maisha yake katika kituo cha
Ushauri nasaha ZAPHA+ mkabala na ofisi ya Halmashauri ya Chake Chake
Pemba.
MKUU
wa Wilaya ya Chake Chake Pemba Mhe:Hanuna Ibrahim Massoud, akimkabidhi
Risala ya wananchi wa Chake Chake Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru
kitaifa Juma Khatib Chum, kwa lengo la Kwenda kumkabidhi Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania.

MKUU
wa Mkoa wa kusini Pemba Mhe:Mwanajuma Majid Abdalla wapili kutoka
kulia, katikati ni Kiongozi wa wakimbizaji wa Mwenge wa Uhuru mwaka huu
Juma Khatib Chum, akifuatiwa na Mkuu wa Wilaya ya Chake Chake Mhe:Hanuna
Ibrahim Massoud akiwa na wakimbizaji wa mwenge wa uhuru pamoja na Mkuu
wa Wilaya ya Mkoani Mhe:Hemed Suleiman Abdalla.

MTOTO
Fatmat Abdalla Mohamed akionyesha hali halisi ya Maisha yake kwa
kutumia mchoro maalimu, tokea alipoanza maisha ya kuishi kwa matumaini
hadi sasa alivyo wakati wa mkesha wa Mwenge wa Uhuru Wilaya ya Chake
Chake.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
Chapisha Maoni