BONDIA Francis Cheka wa Tanzania na Kiatchai Singwancha kutoka
Thailand wamepima uzito leo kwenye ukumbi wa Green Grill uliopo maeneo
ya Victoria jijini Dar es Salaam tayari kwa pambano lao linalosubiriwa
kwa hamu na mashabiki wa Masumbwi.
Pambano hilo litapigwa kesho usiku kwenye ukumbi wa PTA Manispaa ya Temeke.
Cheka na Singwancha watazichapa kwenye pambano hilo la raundi 10
lisilo na ubingwa wowote, lakini ni mabondia hao wawili wanatafuta
kulinda heshima.
Singwancha alitua Dar jana akiongozana na kocha wake tayari kwa
ajili ya pigano hilo ambalo linatarajiwa kuwa na upinzani wa hali ya juu
kutokana na historia ya mabondia wote wawili.
Pambano hilo ambalo litakuwa ni la kwanza kwa Francis Cheka toka
atoke jela linasubiriwa kwa hamu na mashabiki wa ndondi nchini ili kuona
kama ataweza kumsambaratisha Mthailand huyo ambaye ana rekodi nzuri ya
kupiga kwa Technical Knockout (KO).
Cheka amesema kuwa, anataka kuudhihirishia umma wa Tanzania kuwa bado
yuko vizuri kwenye makonde na ili kuthibtisha hilo atashinda pambano
lake kesho, lakini akawaomba wapenzi, mashabiki na wadau wa mchezo wa
ngumi kujitokeza kwa wingi kwa ajili ya kumuunga mkono ili
amsambaratishe mpinzani wake.
“Jela ni jela na ngumi ni ngumi, hakuna chochote kutoka jela
kilichoathiri uwezo wangu wa kupambana ulingoni,watanzania wajitokeze tu
kuja ‘kunisapoti’ ili nimchape mthailand. Wengi wanaujua uwezo wangu
sitai kuzungumza mengi kwenye hilo”, amesema Cheka.
“Ninauhakika wa kushinda kwasababu mimi najua ngumi, ukiwa unajua
kitu unakuwa na uhakika na unachokifanya, kwahiyo watanzania watarajie
ushindi kutoka kwangu”,aliongeza Cheka.
Kwa upande wake Singwancha ametamba kuwa, atashinda kwa kumpiga
Cheka licha ya kukiri kutofahamu uwezo wa bondia huyo ambaye kwa sasa
anatamba kwenye masumbwi hapa Tanzania.
“Sifahamu chochote kuhusu Francis Cheka zaidi ya kusikia jina lake,
sijawahi kumuona akiwa ulingoni. Hilo halinitishi wala kunipa wasiwasi
kwasababunimejiandaa vizuri na ninauhakika wa kushinda pambano hilo la
kesho. Nimefanya mazoezi ya kutosha chini ya kocha wangu na nipo katika
hali nzuri kwa ajili ya kesho”, Singwanchi amesema.
Takwimu za mabondia hao
Francis Cheka
Global ID: 185091
Sex: Male
Birth date: 15 April 1982
Division: Super middle weight
Heght 5’10.5”/ 179 cm
Current weight: 75.7 Kg
Country: Tanzania
Won 30 (KO 16)+Lost 8 (KO 5)+Drawn 2=40
Kiatchai Singwancha
Global ID: 67387
Sex: Male
Birth date: 17 October 1982
Stance: Southpaw
Heght 5’ 7”/ 171cm
Current weight: 75 Kg
Country: Thailand
Won 35 (KO 24)+Lost 12 (KO 9)+Drawn 0=17
Credit:Shaffihdauda
Chapisha Maoni