0


Agizo la kurejesha Magari Millioni 34  hitilafu  limetolewa na Waziri wa Usafirishaji nchini Marekani Bwana Anthony Foxx kufuatia hitilafu ya kiufundi kwenye mifuko ya hewa ya usalama. 

Kampuni inayotengeneza mifuko ya hewa ya usalama ya magari Takata imekiri mifuko ya hewa kulinda usalama wa watumiaji wa magari kuwa na kasoro ambapo baadhi ya mifuko hiyo ya hewa imepasuka kwa nguvu kupita kiasi na kusababisha kurusha vipande vya chuma kwa madereva na abiria wanaokaa viti vya mbele ambapo hadi sasa hitilafu hiyo imesababisha vifo vya watu watano Nchini Marekani.

Magari yanayorejeshwa yanahusu kampuni kumi na moja za kutengeneza magari zikiwemo za Honda, Toyota na Nissan.Urejeshwaji viwandani kwa magari mapya hufanyika baada ya kugundulika hitilafu lolote la kiufundi linaloweza kuhatarisha usalama wa watumiaji wa magari hayo.

Chapisha Maoni

 
Top