Mkuu
wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda akiwa ameubeba mwenge wa Uhuru
baada ya kukabidhiwa na Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi.
Mkuu
wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi (kushoto), akimkabidhi Mwenge wa
Uhuru Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda baada ya kumaliza mbio
zake wilayani humo Dar es Salaam jana asubuhi. Mwenge huo ulianza mbio
zake Wilaya ya Ilala na kuzindua miradi mbalimbali.
Kiongozi
wa mbio za mwenge kitaifa mwaka 2015, Juma Khatibu Chum (kulia),
akisalimia na Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuf Mwenda.
Viongozi
mbalimbali wa Wilaya ya Kinondoni wakiwa wamejipanga katika foleni
wakisubiri kuupokea mwenge wa Uhuru kabla ya kuanza mbio zake wilayani
humo.
Wakimbiza mwenge kitaifa.
Mwenge wa Uhuru ukikimbizwa (kushoto) ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda.
Kiongozi
wa mbio za mwenge kitaifa mwaka 2015, Juma Khatibu Chum akivuta pazia
kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi ya mradi wa maji Mburahati
Barafu na Kisiwani uliofadhiliwa na Jumuia ya Ulaya, Serikali ya
Ubelgiji na Serikali ya Tanzania wakati wa ukimbizaji wa mwenge huo
Wilaya ya Kinondoni humo.
Kiongozi
wa mbio za mwenge kitaifa mwaka 2015, Juma Khatibu Chum akivuta pazia
kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi ya baabara tatu katika Shule ya
Sekondari ya Makulumla. Kulia ni Mkuu wa Shule hiyo, Beatrice Mhina.
Mwanafunzi
Noel Mwita wa Shule ya Sekondari ya Makulumla, akiekeza namna ya
kuchanganya madawa wakati kiongozi huyo wa mwenge, Juma Chum (wa nne
kushoto), alipoweka jiwe la msingi za maabara katika shule hiyo. Kutoka
kushoto ni Mkuu wa shule hiyo, Beatrice Mhina, Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Kinondoni, Camilius Wambura na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul
Makonda
Vijana wa hamasa wa wilaya ya Kinondoni wakitoa burudani mbalimbali wakati wa kuupokea mwenge huo ukitokea wilaya ya Ilala.
Vijana wa hamasa wa wilaya ya Kinondoni wakitoa burudani mbalimbali wakati wa kuupokea mwenge huo ukitokea wilaya ya Ilala.
Wananchi wa Mburahati wakiupokea mwenge huo wakati wa uzinduzi wa mradi wa maji katika eneo hilo.
Vijana wa hamasa wakipamba hafla hiyo kwa kuonesha matukio mbalimbali.
Mwanamuziki
Rehema Chalamila 'Ray C' akitoa ushuhuda wa jinsi alivyoacha matumizi
ya dawa ya kulevya mbele ya Kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa mwaka
2015, Juma Khatibu Chum (hayupo pichani), wakati wa uzinduzi wa kituo
cha vijana walioathiriwa na dawa hizo katika Hospitali ya Mwananyamala.
Kiongozi
wa mbio za mwenge kitaifa mwaka 2015, Juma Khatibu Chum, akimkabidhi
Amina Mshana chandarua kwa ajili ya kujikinga na ugonjwa wa malaria.
Wakimbiza
mwenge wa Uhuru kitaifa, Delina Simfukwe (kushoto) na Bakia Abdallah
wakiteta jambo na mwanamuziki RehemaChalamila 'Ray C baada ya kutoa
ushuhuda kuhusu matumizi ya dawa za kulevya.
Na Dotto Mwaibale
MKUU
wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda ametoa ajira ya moja kwa moja kwa
kijana Yusuf Mzitto mtaalamu wa masuala ya kompyuta ambaye alikuwa
ameathiriwa na matumizi ya dawa za kulevya wa wilaya hiyo.
Makonda
alitoa ajira kwa kijana huyo mbele ya kiongozi wa mbio za mwenge wa
Uhuru mwaka huu. Juma Khatibu Mchum wakati wa uzinduzi wa kituo cha
vijana walioathiriwa na matumizi ya dawa za kulevya kilichozinduliwa na
kiongozi huyo wa mbio za mwenge katika Hospitali ya Mwananyamala Dar es
Salaam jana asubuhi.
"Kijana
huyu mwenye elimu ya juu ya masuala ya kompyuta alikuwa ameathiriwa na
matumizi ya dawa za kulevya hivyo baada ya kuacha kutumia dawa hizo
tumempa ajira katika ofisi yangu ili aweze kufanyakazi badala ya ujuzi
wake kupotea bure" alisema Makonda.
Makonda
alisema kuwa katika kuwawezesha vijana walioathiriwa na dawa hizo
wamepatana na viongozi wa manispaa hiyo kuwa kila kampuni inayofanya
shughuli za kijamii katika wilaya hiyo ili iweze kupata tenda ya kufanya
kazi yoyote ni lazima itoe mchanganuo kwanza wa utoaji wa nafasi ya
ajira kwa vijana wa wilaya hiyo.
Alisema
wamechukua hatua hiyo ili kutoa fursa ya ajira kwa vijana waliohamua
kuachana na matumzi ya dawa za kulevya ambao hawana kazi hivyo kupitia
kakampuni hizo ziweze kuwasaidia vijana hao baada ya kupatiwa tenda na
manispaa hiyo.
Alisema
ili kuunga jitihada za Rais Jakaya Kikwete za kupambana na uingizaji wa
dawa za kulevya ameanzisha mpango wa kukutana mara moja kila mwezi na
vijana walioathiriwa na dawa hizo ili kubadilishana mawazo badala ya
kuwatenga.
Makonda
alisema vijana hao wengi wao ni wataalamu wa masula mbalimbali
akimtolea mfano kijana aliyepewa ajira katika ofisi yake ambaye
atawasaidia katika mambo mengine.
Akizungumzia
mbio za mwenge katika wilaya yake kwa mwaka huu alisema umezindua na
kuweka mawe ya msingi kwenye miradi saba yenye jumla ya sh.5,079,153,972
ambapo kati ya fedha hizo sh.14,802,200 ni fedha kutoka serikali kuu,
sh.2,672,992 kutoka katika Halmshauri ya Manispaa ya Kinondoni,
sh.913,800,780 ni mchango wa wahisani na sh.1,477,978,000 ni michango ya
wananchi.
Alitaja
miradi hiyo kuwa ni pamoja na mradi wa maji, ujenzi wa barabara, ujenzi
wa baabara, ujenzi wa shule za Sekondari, ujenzi wa jengo la wazazi,
ujenzi wa ofisi ya Kata na ujenzi wa nyumba ya walimu.
Alisema
mwenge huo ulipata fursa ya kukagua miradi endelevu wa ugawaji wa
vyandarua, mradi wa wanawake wajasiriamali, mradi wa vijana
wajasiriamali watunzaji wa mazingira na mradi wa huduma za ukimwi.
Kiongozi
wa mbio za mwenge kitaifa Juma Khatibu Chum aliwataka watanzania wote
bila ya kujali itikadi za vyama vyao kudumisha amani na utulivu wa nchi
hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu wa mwezi Oktoba.
Alisema
amani ya nchi tusipo kuwa makini inaweza kuharibiwa kwa siku moja
wakati imetafutwa kwa miaka mingi na aliwata vijana kuacha kutumia dawa
za kulevya na kujikinga ma malaria ambayo yame kuwa yakiua watu wengi
kuliko ukimwi. (Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com)
Chapisha Maoni