Wanaharakati wa haki za binadamu
wanalishutumu Jeshi la Iraq kwa kushindwa kuokoa maelfu ya watu kufikia
sehemu salama ya nchi hiyo mara baada ya wao kukimbia mapigano katika
jimbo la Anbar .
Kwa wale wanaojaribu kuingia Baghdad wanakutana na vikazo vya barabarani katika mitaa ya mji ambapo hatua za kiusalama kwa ajili ya ulinzi zinachukuliwa.
Mwandishi wa BBC amewakuta familia ya Sunni zikiwa zimekwama eneo hilo zikiwa na hali mbaya ambapo wanafikiria kurejea kwenye maeneo yaliyoshikiliwa na IS. Source BBC swahili
Chapisha Maoni