0





 
Saratani aina ya melanoma inayoshambulia ngozi 
Aina ya dawa mbili za kutibu saratani zinaweza kuzuia uvimbe wa saratani kwa watu karibu asilimia 60% wenye saratani iliyofikia kiwango cha juu kijulikanacho kama melanoma, ni kwa mujibu wa majaribio mapya kwa wagonjwa.
Majaribio ya kimataifa yaliyofanyika kwa wagonjwa 945 yalipata tiba kwa kutumia dawa aina ya ipilimumab na nivolumab zikizuia saratani kukua kwa karibu mwaka mmoja kwa wagonjwa asilimia 58%.
Madaktari wa Uingereza waliwasilisha data hizo kwa chama cha madaktari wa Marekani.
Taasisi ya Utafiti wa Saratani nchini Uingereza kiesema dawa hizo zinatoa tiba kali dhidi ya aina moja ya saratani hatari.
Melanoma, hatua ya hatari ya saratani ya ngozi, ni aina ya sita ya saratani ya kawaida nchini Uingereza. Inaua zaidi ya watu 2,000 kila mwaka nchini humo.

Chapisha Maoni

 
Top