Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Jumuiya ya
Afrika Mashariki, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (wa kwanza kulia) kwa
pamoja na Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museven (wa pili kulia), Rais wa
Afrika Kusini, Mhe Jacob Zuma (wa tatu kutoka kulia), Waziri wa Mambo ya
Nje wa Burundi, Mhe. Alain Nyamitwe (wa tatu kushoto) na Katibu Mkuu wa
Jumuiya ya Afrika Mashariki, Dkt. Richard Sezibera (wa pili kushoto),
wakiimba wimbo wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, kabla ya kuanza rasmi kwa
Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki
kujadili hali ya siasa na usalama nchini Burundi. Mkutano huo ulifanyika
Ikulu, Dar es Salaam tarehe 31 Mei, 2015.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,
Balozi Liberata Mulamula (wa pili kutoka kulia) akifuatiwa na Katibu
Mkuu wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bibi Joyce Mapunjo na
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje (kulia) nao wakiimba wimbo
wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Dkt. Richard Sezibera akisoma maazimio yaliyofikiwa mara baada ya
Mkutano wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kumalizika.
Kundi la Watu Maalum la Jumuiya ya Afrika Mashariki linalofuatilia
hali ya siasa na usalama nchini Burundi chini ya uongozi wa Waziri Mkuu
Mstaafu wa Tanzania, Jaji Joseph Sinde Warioba wakifuatilia mkutano wa
Wakuu wa Nchi wa EAC. Kulia ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Afrika Kusini.
Juu na Chini ni Wajumbe mbalimbali wakifuatilia mkutano wa wakuu wa nchi wa EAC
Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini, Mhe. Radhia Msuya (katikati)
akiwa pamoja na Mkurugenzi Msaidizi katika Ubalozi wa Tanzania nchini
Burundi, Bibi Victoria Mwakasege nao wakifuatilia mkutano
Maafisa Mambo ya Nje nao wakifuatilia kwa makini mkutano
Sehemu ya Mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini nao wakifuatilia mkutano
Mkurugenzi wa Idara ya Habari, Bw. Assah Mwambene (katikati) kwa
pamoja na Afisa Habari wa Sekretarieti ya Maziwa Makuu Bw. Macdonald
Mwakasendile (kushoto) wakirekodi matukio
Rais Kikwete akifuraia jambo na Rais wa Afrika Kusini Mhe. Zuma
pamoja na Rais wa Uganda Mhe. Museveni mara baada ya kumaliza mkutano.
Rais Kikwete akizungumza jambo na Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa
Afrika, Bi.Nkoosazana Dlamini-Zuma kabla ya kuanza mkutano.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard
Membe akiongozana na Rais wa Kenya, Mhe. Uhuru Kenyatta tayari kwenda
kuanza mkutano wa kujadili hali ya usalama nchini Burundi .
Katibu Mkuu wa Mambo ya Nje, Balozi Liberata Mulamula akizungumza jambo na Mwakilishi wa Umoja wa Ulaya,, Bw. Vervaeke.
....Kuwasili kwa viongozi wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje Balozi Mulamula akisalimiana na Rais wa Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta
Rais wa Kenya Mhe. Uhuru Kenyetta akipita kwenye Gwaride la Heshima mara baada ya kuwasili nchini
Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Harrison Mwakyembe
akimtambulisha Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na UShirikiano wa
Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula kwa Rais wa Uganda mara baada ya
kumpokea Rais huyo alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
Julius Nyerere.
Rais Museven akipita katikati ya Gwaride la heshima.
Balozi wa Tanzania nchini Afrika ya Kusini Balozi Radhia Msuya akisalimiana na Rais wa Afrika ya Kusini alipowasili nchini
Picha ya Pamoja baada ya Mkutano wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki
Picha na Reginald Philip
Chapisha Maoni