Mshirikishi mkuu wa shirika la Umoja wa mataifa nchini Sudan Kusini,
Toby Lanzer, amesema kuwa takriban watoto laki mbili u nusu wamo katika
hatari ya kufa katika kipindi cha miezi kadhaa ijayo iwapo mashirika ya
utoaji misaada, hayatafikisha misaada kwa watu walio na mahitaji.
Bwana Lanzer ameiambia BBC kuwa, watu wanateseka kwa sababu ya umaskini.
Vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Sudan Kusini imesambaratisha uchumi wa taifa hilo.
Amesema kwamba mashirika ya utoaji misaada yatafanya yawezavyo
kuwasaidia wahitaji, lakini amani itapatikana tu nchini Sudan Kusini
iwapo viongozi watakubaliana kukomesha mapigano.
Bwana Lanzer amewasihi viongozi wa pande hasimu kusameheana ilikukomesha maafa.
BARAZA LA WAFANYAKAZI OFISI YA MWANASHERIA MKUU LAKUTANA
-
• Mwanasheria Mkuu wa Serikali asisitiza kuendelea kusogeza huduma karibu
na Wananchi
Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali li...
Saa 5 zilizopita
Chapisha Maoni