Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma, alitoa maelezo katika mkutano wa AU siku ya Ijumaa na kuhimiza nchi za Afrika kujihuisha na ukuzaji wa raslimali zake za madini badala ya kutegemea wawekezaji kutoka nchi za kigeni.
Zuma alisema, ‘’Tumekubaliana kama viongozi kwamba hatutoruhusu raslimali zetu za madini tunazozimiliki kukuzwa nje ya bara la Afrika. Shughuli zote za utengenezaji na ukuzaji zinapaswa kufanyika ndani ya Afrika ili kuweza kuwafaidisha watu wetu wa Afrika.’’
Wakati huo huo, Zuma pia alishiriki mashindano ya AU Presidential Golf Challenge yaliyolenga kuchangisha fedha kwa ajili ya miradi ya AU.
Zuma alitoa shukrani kubwa kwa wajumbe waliohudhuria
mkutano wa AU na kudhihirisha furaha yake aliyokuwa nayo kwa kupata
fursa ya kuandaa mkutano huo muhimu nchini Afrika Kusini. CHANZO TRT SWAHILI
Meya Kigamboni awafariji wagonjwa agawa zawadi
-
Na MWANDISHI WETU
Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni ambaye ni Diwani wa
Kata ya Kibada Mhe. 𝗔𝗺𝗶𝗻𝗶 𝗠𝘇𝘂𝗿𝗶 𝗦𝗮𝗺𝗯𝗼, amefanya ...
Saa 3 zilizopita
Chapisha Maoni