Mwili wa aliyekuwa kiongozi wa karibu wa Saddam Husein Tareq Aziz, umewasili katika mji mkuu wa Amman nchini Jordan.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa familia na baadhi vyanzo vya habari, jeneza la Tareq Aziz lilidaiwa kutoroshwa na kundi moja la watu waliojihami kwa silaha.
Serikali ya Iraq imekanusha madai hayo na kusema kwamba jeneza hilo lilisubirishwa Baghdad kwa muda kutokana na baadhi ya taratibu zilizokuwa zikifuatiliwa.
Waziri Mkuu wa Iraq Haydar Abadi, alitoa idhini ya kuwasilishwa kwa jeneza la Tareq Aziz kwa familia yake nchini Jordan pasi na kufanyiwa sherehe wala maandamano ya aina yoyote.
Tareq Aziz ambaye ni waziri wa zamani wa mambo ya nje wa Iraq
na aliyewahi kuhudumu kama naibu waziri mkuu wakati wa utawala wa
Saddam Husein, alifikishwa hospitalini kutoka kwenye gereza alilofungwa
na kupoteza maisha tarehe 5 mwezi Juni akiwa na umri wa miaka 79. CHANZO: TRT SWAHILI
MHANDISI JOANES AWATAKA OLCHORONYORI KUWA MABALOZI WA KUKABILIANA NA
MABADILIKO YA TABIANCHI
-
Na Mwandishi wetu, Simanjiro
HALMSHAURI ya Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, baada ya kupata mradi wa
mpango wa kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi (S...
Saa 5 zilizopita
Chapisha Maoni