Watalii wanne wameripotiwa kutozwa faini kwa kosa la utovu wa nidhamu baada ya kukamatwa wakiwa wamejianika uchi juu ya kilele cha mlima wa Kinabalu nchini Malaysia.
Watalii hao wanne ambao wawili wamebainishwa kuwa
raia wa Canada, mmoja wa Uingereza na mwingine mmoja wa Uholanzi,
waliwabughudhi wananchi wa Malaysia kwa kujianika uchi juu ya kilele cha mlima Kinabalu.
Kitendo hicho cha utovu wa nidhamu kinaaminika
kuudhi mapepo ya mlima Kinabalu na kusababisha maafa ya tetemeko la
ardhi lililopelekea vifo vya watu 18 siku ya Ijumaa.
Watalii wote wanne walitakiwa kuchagua kati ya kulipa faini ya fedha dola 1,330 au kufungwa miezi mitatu gerezani iwapo watashindwa kulipa faini hiyo.
Uamuzi huo ulitoalea baada ya watalii hao kufungwa kwa siku tatu tangu siku ya Jumatano. Watalii hao pia wanatarajiwa kutimuliwa kutoka nchini humo. CHANZO: TRT SWAHILI
NMB yajivunia ushiriki, udhamini wa matukio Sherehe za Mapinduzi Z’bar
-
NA MWANDISHI WETU, ZANZIBAR
WAKATI Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) ikiitunukia Cheti cha Shukrani
na Pongezi kwa kufadhili, kudhamini na kushiriki ...
Saa 1 iliyopita
Chapisha Maoni