Kama uko karibu sana na TV za Kimataifa kama BBC, Sky News na CNN utagundua
kwamba kwenye stori kubwa zilizopewa headlines sana iko ya Shambulio la
Kugaidi lililotokea Tunisia na kusababisha mauaji ya Watalii.. Breaking News imeingia
nayo kwenye stori kubwa zilizo kwenye headlines sasahivi, inahusu Ndege
ya Kijeshi kuanguka kwenye makazi ya watu Indonesia na watu
30 wamefariki.
Ndege hiyo ilipata ajali muda mfupi baada ya kuruka kutoka kwenye Uwanja wa Medan Polonia Airport..
ndani ilikuwa imebeba jumla ya watu 113, ndege imeanguka kwenye mtaa
ambao una makazi ya watu pamoja na Hoteli, gari moja pia limewaka moto
baada ya kutokea ajali hiyo.. eneo lote la ajali limeshika moto.
Wenyeji
wa eneo hilo wamesema hii ni mara ya pili kwa nyumba za eneo hilo
kuangukiwa na ndege, iliwahi kuanguka Boeing 737 mwaka 2005 ikaua watu
143 na kati yao watu 30 walikuwa ni watu ambao wanaishi eneo hilo,
hawakuwemo ndani ya ndege.
Vikosi
vya Zimamoto na Uokoaji vinaendelea na kazi ya kuzima moto pamoja na
kutoa miili ya watu waliofariki kwenye ajali hiyo, huenda idadi ya
waliofariki na majeruhi ikaongezeka wakati wowote kuanzia sasa.
Chapisha Maoni