Ikiwa mihula miwili ya rais Barack Obama ikielekea ukingoni, Ben Carson
ambae ni daktari mstaafu wa tiba ya mishipa amejitangaza kuwa atawania
kiti cha urais katika uchaguzi utakaofanyika nchini Marekani ifikapo
mwaka 2016.
Ben Carson ni mzawa wa jimbo la Detroit, jimbo ambalo linapatikna kaskazini magharibi mwa Marekani, alihitimu katika chuo kikuu cha Ivy League Yale na chuo kikuu cha Michigan.
Ben Carson ana umri wa miaka 64.
Daktari mtaalamu wa tiba ya mishipa, Ben Carson aliongoza kundi la madaktari 70 waliofaulu kuwaachanisha mapacha waliozaliwa wameshikana vichwa.
Ben Carson alikiambia kituo cha televisheni cha Fox News kuwa iwapo atachaguliwa, kodi itakuwa ikitolewa kwa misingi ya biblia "fungu la 10".
Baada ya mihula miwili ya Barack Obama, Ben Carson atachaguliwa kuwa rais wa 45 wa Marekani ?
CHANZO TRT SWAHILI
IAA KUBORESHA MAZINGIRA YA KUJIFUNZIA ILI KUENDELEA KUZALISHA WATAALAM
MAHIRI
-
Na Mwandishi Wetu
MKUU wa Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA), Prof. Eliamani Sedoyeka amesema IAA
itaendelea kuimarisha miundombinu na mazingira ya kujifunz...
Saa 14 zilizopita
Chapisha Maoni