Kiril Gaburici, aliyeanza kuhudumu kama waziri mkuu nchini Moldova tarehe 18 mwezi Machi mwaka 2015, ameripotiwa kujiuzulu.
Gaburici alitoa maelezo kwa vyombo vya habari na kutangaza kujiuzulu baada ya kukabiliwa na kesi ya kumiliki vyeti bandia vya elimu.
Gaburici alisisitiza kwamba madai hayo ya umiliki wa vyeti bandia vya elimu ni mbinu ya michezo ya kisiasa inayotumiwa dhidi yake.
Gaburici alisema, ‘’Natumai baada ya kujiuzulu
kwangu, tetesi za vyeti vyangu zitaisha na masuala mengine muhimu zaidi
yanayokumba jamii yataangaziwa.’’
Wiki iliyopita, Gaburici alitoa maelezo kupitia
mtandao wa ofisi ya waziri mkuu na kuwataka baadhi ya viongozi wakuu wa
halmashauri kama za nchi kujiuzulu kutokana na madai ya ufisadi.
Gaburici pia alifahamisha kwamba atachukuwa hatua ya kujiuzulu endapo ombi lake halitotiliwa maanani.
Baada ya maelezo hayo, Gaburici mwenye umri wa miaka 38, alianza kuandamwa na kesi za umiliki wa vyeti bandia. CHANZO TRT SWAHILI
RAIS WA BURUNDI AMFARIJI RAIS SAMIA KIZIMKAZI ZANZIBAR
-
Rais wa Jamhuri ya Burundi, Mhe. Evariste Ndayishimiye, akimfariji Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, nyumbani
kwake...
Siku 1 iliyopita
Chapisha Maoni