Serikali ya Burundi imesema
haitashiriki katika mazungumzo yaliyodhaminiwa na Umoja wa Mataifa
yakilenga kupunguza hali ya uhasama uliopo kabla ya kufanyika kwa
uchaguzi wenye utata.
Maandamano yamekuwa yakiendelea kwa wiki kadha kupinga hatua ya Rais Pierre Nkurunziza kutaka kuwania nafasi ya urais kwa mara ya tatu.
Viongozi wawili katika serikali ya Rais Nkurunziza - akiwemo mmoja wa makamu wa rais, Gervais Rufyikiri, na spika wa bunge la nchi hiyo, Pie Ntavyohanyuma, wamekimbilia Ubelgiji.
Wote wawili wamekuwa wakosoaji wa rais. Uchaguzi umepangwa kufanyika mwezi uajao. Uchaguzi wa wabunge unafanyika Jumatatu.
Gervais Rufyikiri aliyekuwa makamu wa rais wa Burundi amekimbilia Ubelgiji.
Chapisha Maoni