0
Nigeria : "Seneti yenye mshahara mkubwa duniani"

Wawakilishi wa baraza la Seneti na wabunge wa Nigeria miongoni mwa wabunge wanaolipwa kitita kikubwa cha pesa ulimwenguni

Nchini Nigeria kumeanzishwa kampeni iitwayo Open NASS katika mitandao ya kijamii inayokemea mishahara mikubwa wanayopokea wawakilishi wa baraza la seneti.

Kampeni hiyo inaomba ufafanuzi kuhuzu mishahara hiyo ambayo inesemekana kuwa mikubwa mno.
Wabunge na wanaseneti nchini Nigeria hupokea Euro 12,000 kwa  mwezi.

Kitita hicho cha mshahara kinapeleka Nigeria kushikilia nafasi ya kwanza barani Afrika ya wabunge wanopokea mshahara mkubwa.

Kitita hicho kiliweka bunge la Nigeria katika orodha ya wabunge wanaopokea mishahara mikubwa duniani kama vile Ufaransa, Uswidi, Israel na Uingereza.

Kwa mwaka hujikusanyia kitita kikubwa cha pesa kushinda kile ambacho hukusanya waziri mkuu wa Uingereza.

Rais Muhammadu Buhari ambae amechaguliwa siku za nyuma, yeye hupokea takriban sarafu za Ulaya 5,000.Nchini Nigeria kiwango cha chini cha mshahara kwa mwezi ni pesa 81 sarafu za Ulaya.TRT SWAHILI

Reuters

Chapisha Maoni

 
Top