Eto'o ambaye amewahi kuwa mchezaji bora wa Afrika kwa mara nne na kuwa mchezaji wa tatu bora wa FIFA mwaka 2005, anatinga kucheza katika ligi ya tano.
Kabla ya hapo, Eto'o amewahi kucheza katika ligi za nchi za Uingereza, Hispania, Italia na Urusi kabla ya kujiunga na Antalyaspor ya Uturuki.
Uhamisho huo wa Eto'o umegusa vichwa vingi vya habari katika magazeti na mitandao ya kijamii barani Ulaya na duniani kwa ujumla.
Kwasasa, Eto'o tayari ameshatua jijini Antalya kwa ajili ya klabu yake hiyo mpya. Nyota huyo wa zamani wa Chelsea ameshamaliza majaribio ya kiafya na kuidhinishwa kuwa mchezaji wa timu hiyo ya Antalyaspor.
Chapisha Maoni