0
28 wafariki kwa mafuriko China

Watu 28 waripotiwa kupoteza maisha kutokana na mvua kali, zilizopelekea mafuriko na mmomonyoko wa ardhi China

Takriban watu 28 wafariki na wengine hawajulikani walipo kufuatia mvua kali zinazonyesha kwa muda wa siku 4 na kupelekea mafuriko na mmomonyoko wa ardhi nchini China.

Shirika la habari la Shangcheng kutoka mji wa Henan, lilifahamisha kuwa watu watano wanaripotiwa kufa na wengine 800 walihama miji yao huku majengo 100 kuharibika na zaidi ya 200 kujeruhiwa.

İnafahamishwa kutokea kwa hasara ya kiuchumi ya Yuan milion 305, na uharibifu wa hekta 6,700 za mazao na uharibifu wa maguzo ya umeme.

Katika mji wa Shaanxi, wameripotiwa vifo vya watu 4 na wegine 9 hawajulikani walipo, na kupata hasara ya Yuan milioni 170 ikiwa ni pamoja na kuharibika kwa nguvu za umeme.

Wakati huo huo, watu wawili wameripotiwa kufa siku ya Jumatatu kufuatia mafuriko hayo na maporomoko ya ardhi katika jimbo hilo la Anhui Jinzhai, wakati wengine watano hawajulikani walipo.

Chapisha Maoni

 
Top