Zaidi ya watu 11 wafariki katika ajali ya ndege İndonezia
Msemaji wa jeshi Fuad Basya, amefahamisha katika kituo cha televisheni ya Metro kuwa miili mitano ndio imekwisha fikishwa hospitali.
Aliendelea kufahamisha kuwa aina ya ndege ya Hercules ilikuwa imebeba wafanyakazi 12 wakati ilipopata ajali muda mfupi baada ya kuanza safari katika uwanja wa ndege wa Soewondo mida ya saa 6 na dakika 8 mchana.
Basya alilifahamisha shirika la habari la anadolu kuwa chanzo cha ajali hiyo bado hakijafahamika.
Ndege hiyo ilikuwa ikielekea mji wa Tanjung Pinang katika kisiwa cha Riau.
Shahidi mmoja ambaye alifahamika kwa jina la Guntur amefahamisha mtandao wa kijamii wa Kompas.com kuona moshi moshi mkubwa katika eneo la tukio.TRT SWAHILI
Chapisha Maoni