0
DRC : Rais Kabila atoa wito wa mazungumzo

Rais Joseph Kabila atao wito wa mazungumzo bila ushirikiano wa kimataifa

Rais wa Jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo, Joseph Kabila ametoa wito wa mazungumzo baina ya wakongomani wenyewe bila kuingiliwa kati.

Wito huo umetolewa baada ya upinzani kuomba mazungumzo na wawakilishi wa kimataifa.
Katika sherehe za kuazimisha maika 55 ya uhuru wa Jamuhuri ya Kidemokrasia, rais Kabila alifahamisha kuwa alitilia maanani ombi la upinzani kuhitaji mazungumzo na serikali.

Rais Kabila alifahamisha kuwa yupo tayari kwa mazungumzo ila bila ushirikiano wa kimataifa.
Upinzani nchini humo ulifahamisha kuwa katika mazungumzo hayo ni muhimu kuepo na wawakilishi wakimataifa.TRT SWAHILI

Chapisha Maoni

 
Top