Harusi ya
mshambuliaji wa Simba, Mganda Emmanuel Okwi imeacha historia nchini
Uganda akitumia dola 80,000 ( Sh 160,000 Mil ) kwa ajiri ya kuifanikisha
iliyofanyika Jumamosi jijini Kampala.
Kiasi
hicho kinatosha kabisa kukamilisha usajili wa timu zisizopungua tatu za
Ligi Kuu Bara, lakini yeye alitumia fedha hizo kwa ajili ya sherehe,
huku Gazeti hili lilikuwa Uganda na kushuhudia kila kitu kilivyokuwa
kinaendelea wakati Okwi akimuoa Florence Nakalega.
Mshambuliaji
wa zamani wa Yanga, Hamis Kiiza na Nabisubi Julian ndiyo walikuwa
wasimamizi wao wa harusi hiyo, ilifungwa katika kanisa la Miracle Centre
Cathedral lililopo Lubaga, Kampala.
Baada ya
hapo shughuli ya kupiga picha za ukumbusho kwa maharusi, ilifanyika
katika hoteli kubwa ya kifahali ya Munyonyo Lesort Beach na kumaliziwa
na sherehe kamili kwenye Ukumbi wa Main Exbition Hall uliopo ndani ya
jengo la UMA maeneo ya Lugogo.
Okwi alitumia magari saba yalikuwa maalumu kuwabeba maharusi, kati ya hayo matano ni aina ya Jaguar na mawili Brevis.
Hata
hivyo, msafara wa harusi hiyo ulipata matatizo baada ya magari mawili
yaliyowabeba wasimamizi akiwemo Hamis Kiiza kupata ajali, lakini hakuna
aliyeumia zaidi ya mishtuko ya kawaida.
Maharusi wabadili nguo mara mbili
Hapa
ndipo kulikuwa na utamu kamili, maharusi waliingia ukumbini majira ya
saa 11 jioni, mwanaume walivaa suti za bluu na mwanamke gauni na shela
nyeupe kabla ya kwenda kubalisha na kuvaa suti za kaki kwa wanaume na
bibi harusi alivaa gauni lenye rangi ya kijivu.
Okwi
alipokelewa na wachezaji wenzake waliokuwa wameshika mipira kwa juu yeye
akapita katikati yao huku wakicheza na baada ya hapo walikabidhiwa
mpira na makocha Sam Simbwa na Moses Basena.
Katika
hali isiyo ya kawaida, Okwi alijikuta akidondosha chozi alipokuwa
anazungumzia wasifu wa mkewe, Florence na alilia baada ya kuona chozi la
mkewe ambaye ndiye alianza kuelezea wasifu wa mumewe.
Okwi alipoulizwa alisema: “Nililia kutokana na furaha kwani tumepita katika mazingira ya kila namna, magumu na raha.
“Nimefurahi
sana kukamilisha shughuli hii na sasa nina mke ambaye tutatengeneza
familia moja na atakuwa mshauri wangu,” alisema Okwi.
Chapisha Maoni