Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Ernest Mangu akikagua Gwaride
Maalum lililoandaliwa na Wahitimu wa Mafunzo ya Uongozi wa Magereza
Daraja la Pili ambayo yamefungwa rasmi leo Juni 22, 2015 katika Chuo cha
Maafisa Magereza Ukonga, Jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Ernest Mangu akimvisha cheo cha
Mkaguzi Msaidizi wa Magereza Mhitimu wa Mafunzo ya Uongozi wa Magereza
Daraja la Pili ambaye amefanya vizuri kwa upande wa Gwaride, Stafu
Sajini Boniphace Felix. Mhitimu huyo amevishwa cheo hicho kwa niaba ya
Wahitimu 216 wa Mafunzo hayo.
Wahitimu wa Mafunzo ya Uongozi wa Magereza Daraja la Pili wakipita
mbele ya Mgeni rasmi IGP Ernest Mangu(hayupo pichani) katika mwendo wa
haraka wakitoa heshima leo Juni 22, 2015 katika Chuo cha Maafisa
Magereza Ukonga. Jumla ya Wahitimu 216 wamehitimu Mafunzo
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Ernest Mangu akipokea Salaam ya
heshima kutoka kwa Gwaride lililoandaliwa na Wahitimu wa Mafunzo ya
Uongozi Daraja la Pili(kushoto katika Jukwaa) ni Kamishna Jenerali wa
Jeshi la Magereza, John Casmir Minja.
Maafisa wa Jeshi la Magereza wakionyesha umahiri mkubwa wa mbinu
mbalimbali za kujihami na adui kama wanavyoonekana kikakamavu katika
picha wakati wa hafla fupi ya kufunga Mafunzo ya Uongozi Daraja la Pili.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja(kulia)
akifurahia onesho Maalum la Maafisa wa Jeshi la Magereza kutoka Kikosi
Maalum cha Kutuliza Ghasia Magerezani(katikati) ni Mkuu wa Jeshi la
Polisi Nchini, IGP Ernest Mangu(kushoto) ni Kamishna Mkuu wa Idara ya
Uhamiaji, Sylivester Ambokile wakifurahia onesho hilo kama
wanavyoonekana katika picha.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja akitoa
maelezo mafupi kabla ya kumkaribisha Mgeni rasmi kufunga Mafunzo ya
Uongozi Daraja la Pili kwa Maafisa wa Jeshi la Magereza.
Kikundi cha kwaya kinachoundwa na Maafisa wa Jeshi la Magereza wa
Chuo cha Maafisa Magereza, Ukonga kikitumbuza mbele ya Mgeni rasmi, IGP
Ernest Mangu(hayupo pichani)katika sherehe za kufunga Mafunzo hayo ya
Uongozi Daraja la Pili, Chuo cha Maafisa Magereza Ukonga.
Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza wakifuatilia kwa umakini
matukio mbalimbali katika sherehe hizo za kufunga Mafunzo ya Uongozi
Daraja la Pili(wa kwanza kushoto) ni Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa
Magereza, Dkt. Juma Malewa(katikati) ni Kamishna wa Huduma za
Urekebishaji, Deonice Chamulesile(kulia) ni Mkuu wa Chuo cha Maafisa
Magereza Ukonga, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Erasmus Kundy(Picha zote
na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).
Chapisha Maoni