Katibu Mkuu wa
CCM Ndugu Abdulrahman Kinana pamoja na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi
Nape Nnauye wameongoza makundi ya vijana kutoka Shirikisho la Vyuo Vikuu
pamoja na Machinga wa mjini Mwanza kukimbia mchakamchaka (jogging) kwa
umabali wa kilomita 8,kuanzia Barabara ya Stesheni,kupitia barabara ya
Posta,Kenyatta, Karuta,Lumumba maeneo ya Soko Kuu mpaka Stendi ya zamani
Tanganyika. Viongozi mbali
mbali walishiriki mchakamchaka huo akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.
Magessa Mulongo,Mbunge wa Jimbo la Kwimba Mhe. Shanif Masoor na Katibu
wa CCM mkoa wa Mwanza Ndugu Miraji Mtaturu.
Katibu Mkuu wa
CCM Ndugu Abdulrahma Kinana akikimbia mchaka mchaka (jogging)katika
mitaa ya jiji la Mwanza ,wengine pichani ni Katibu wa CCM wilaya ya
Nyamagana Mpanda(kushoto),Katibu wa CCM mkoa wa Mwanza Ndugu Miraji
Mtaturu na wa mwisho kulia ni Mwenezi wa CCM mkoa wa Mwanza Magelepa.
Katibu Mkuu wa
CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na vijana walioshiriki
mchakamchaka (jogging) na kuwataka kuendelea kufanya mazoezi kwani
yanasaidia kuimarisha afaya na kujenga mwili.
Chapisha Maoni