Katibu
Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akiwasili kuhutubia mkutano wa hadhara
aliofanya katika Viwanja vya CCM, wilaya ya Sengerema mjini, akiwa
katika ziara ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM na Uhai wa Chama
mkoani Mwanza, leo.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia maelfu ya wananchi
waliojitokeza katika mkutano wa hadhara aliofanya katika viwanja vya
Ofisi ya CCM, wilaya ya Sengerema mjini, akiwa katika ziara ya kukagua
utekelezaji wa ilani ya CCM na Uhai wa Chama mkoani Mwanza leo
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye akuhutubia mkutano wa
hadhara ya Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana uliofanyika leo na
kuhudhuriwa na maelfu ya wananchi, katika viwanja vya CCM wilaya ya
Sengerema mjini.
Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja, akieleza alivyoshiriki katika
utekelezaji wa ilani ya CCM, alipohutubia mkutano wa katibu Mkuu wa CCM
Abdulrahman Kinana uliohudhuriwa na maelfu ya wananchi katika Viwanja
vya Ofisi ya CCM wilaya ya Sengerema mjini leo.jioni
Wananchi waliofurika katika Uwanja wa Ofsi ya CCM wilaya ya Sengerema
mjini, wakishangilia wakati wa mkutano wa Katibu Mkuu wa CM Abdulrahman
Kinana uliofanyika kwenye viwanja hivyo leo jioni
Mkuu wa mkoa wa Mwanza Magesa Mulongo akihutubia maelfu ya wananchi
katika mkutano wa Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana uliofanyika leo
kwenye viwanja vya CCM wilaya ya Sengerema mjini.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiteta jamb na Mkuu wa mkoa
wa Mwanza Magesa Mulongo wakati wa mkutano wake wa hadhara uliofanyika
leo katika Viwanja vya Ofisi ya CCM wilaya ya Sengerema mjini.
"Naam mkutano wetu umefanikiwa" inaelekea ndivyo alivyokuwa akiwaza
huku akitabasamu, Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana wakati wa
mkutano wake wa hadhara aliofanya leo, kwenye Viwanja vya CCM wilaya ya
Sengerema mjini.
ALIPOKAGUA MIRADI YA MAENDELEO KABLA YA MKUTANO HUO
"Kwa hiyo mradi huu ndiyo umekwamia palee, siyo", Katibu Mkuu wa CCM
Abdulrahman Kinana akimuuliza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya
Serengeti, Mathew Lubongeja, alipokagua mradi wa Kilimo cha Skimu,
Katunguru, alipokagua mradi huo akiwa katika ziara ya kukagua
utekelezaji wa ilani ya CCM na uhai wa Chama, katika Jimbo la Sengerema
mkoani Mwanza. Mradi huo ambao ni mkubwa umekwama kumalizika kwa madai
ya kukosa fedha baada ya kutumia sh. milioni 700 tu, kati ya Shilingi
Bilioni 2 zilizokuwa zimekadiriwa kumaliza mradi huo. Kwa mujibu wa
Mkurugenzi huyo, fedha hizo zinatakiwa kutolewa na serikali.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (kulia), na msafara wake
wakipita kwenye moja ya matuta ya mradi huo ambao umekwama kumalizika.
Risala aliyosomewa Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana wakati alipokagua mradi huo.
AKIKAGUA SOKO LA HALMASHAURI YA SENGEREMA
Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akikagua hali ya Soko Kuu la
Halmashauri ya mji wa Sengerema, akiwa katika ziara ya kukagua
utekelezaji wa ilani ya CCM na uhai wa Chama mkoani Mwanza leo. Soko
hilo limelalamikiwa na watumiaji kuwa na uchafu uliokithiri katika
maeneo mbalimbali vikiwemo vyoo.
Vijana wakimuonyesha Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana hali
ilivyo mbaya katika moja ya mabucha kutokana na jengo kwenye soko hilo
kuvuja nyakati za mvua
Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akitazama mtaro wa maji taka kwenye soko hilo
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana aitazama maji machafu yanavyotiririka hovyo kutoka kwenye vyoo
Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akimhoji Mbunge wa Sengerema,
William Ngeleja kujua imekuwaje hadi hali ya soko kuwa mbaya, alipokagua
vyoo na kushuhudia hali mbaya
Kinana akizungumza na wananchi baada ya kukagua kivuko hicho
Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana wakienda kuingia kwenye Kivuko hicho kabla ya uzinduzi
Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akikata utepe kuzindua Kivuko hicho
Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akisaini kitabu baada ya kuzindua kivuko hicho
Taswira ya kivuko hicho cha Kisasa
Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman kinana akizindua jiwe la msingi ujenzi
wa Ofisi ya CCM wilaya ya Sengerema akiwa katika ziara ya kukagua
utekelezaji wa ilani ya CCM na uhai wa Chama mkoani Mwanza
Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akikagua ujenzi tangi na chujio
la maji la mradi wa maji wa Sengerema mjini uliopo eneo la
Nyamazugowa, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM
na uhai wa Chama mkoani Mwanza, leo. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO-CCM
Blog
Chapisha Maoni