Maafisa wa usalama nchini Misri
wanasema kuwa shambulio katika mji mkuu, Cairo, limemjeruhi kiongozi wa
mashtaka, Hisham Barakat.
Shambulizi hilo linafanyika baaada ya kundi linaloshirikishwa na Islamic state huko Misri kuitisha mashambulizi baada ya hukumu ya mahakama kutolewa kuwa wapiganaji sita wanyongwe.
Bwana Barakat amekuwa akipendekeza mamia ya wapiganaji hao kufunguliwa mashtaka tangu kupinduliwa kwa rais aliyependuliwa , Mohamed Morsi, mwaka 2013.BBC SWAHILI
Chapisha Maoni