Serikali ya Ugiriki imethibitisha
kuwa benki zake zitafungwa kwa kipindi cha juma moja kufuatia uamuzi wa
Benki kuu barani Ulaya wa kutoendelea kutoa fedha za kukabiliana na
dharura.
Katika hotuba iliopeperushwa na runinga za taifa hilo Waziri mkuu nchini Ugiriki Alexis Tsipras ameomba utulivu.
Mwandishi wa BBC mjini Athens amesema kuwa hakuna ishara za wasiwasi huku raia wakionekana kuelekea makazini kama kawaida.
Hatua hiyo ya benki kuu ya Ulaya inafuatia kuanguka kwa mazungumzo katika ya Ugiriki na mataifa ya Ulaya kuhusu makubaliano yanayokwisha siku ya jumanne ya kulikwamua taifa hilo kutoka kwa madeni yake,siku ambayo taifa hilo linafaa kulipa Hazina ya fedha duniani dola bilioni 1.6.
Chapisha Maoni