0

Waziri mkuu nchini Uingereza David Cameron amesema kuwa wapiganaji wa islamic state ni tishio kubwa mataifa ya magharibi.

Bwana Cameron amesema kuwa wapiganaji wa Islamic state nchini Syria na Iraq wamekuwa wakipanga mashambulizi dhidi ya Uingereza na kwamba vita dhidi yao vitakuwa 'mapambano ya kizazi chetu'.
Ameapa kutekeleza mashambulizi makali dhidi ya kundi hilo la jihad.

Matamshi ya bwana Cameron yanajiri baada ya kubainika kuwa takriban watalii 38 waliuawa siku ya ijumaa katika eneo moja la mapumziko nchini Tunisia. BBC SWAHILI

Chapisha Maoni

 
Top