Askari
wa Polisi wakiwa katika gari na baadhi ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha
Kampala (KIU) waliowakamata katika maandamano hayo.
Rais
wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Kampala (KIUPESO),Elias
Mbogho akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya
maandamano yaliyofanyika leo katika hicho jijini Dar es Salaam,Kushoto
ni Makamu wa Rais wa Serikali ya Wanafunzi,Jamal Mohamed.

Wanafunzi wa KIU wakiwa na mabango yenye ujumbe mbalimbali.

Kikosi cha kutuliza ghasia (FFU) wakiwa kazini leo katika Chuo Kikuu cha Kampala jijini Dar es Salaam.

Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Kampala akiwa na majeraha katika maandano yaliyofanyika katika chuo hicho jijini Dar es Salaam.

Wanafunzi wakiwa katika maandamano katika Chuo Kikuu cha Kampala leo jijini Dar es Salaam.PICHA NA EMMANUEL MASSAKA.
Na Chalila Kibuda
Wanafunzi
wa Chuo Kikuu cha Kimataifa Cha Kampala (KIU) leo wameandamana na
katika chuo hicho kushinikiza warudishe fedha zao kutokana na kuanzisha
kitivo ambacho hakitambuliki na mamlaka za nchi.
Mgomo
huo umeanza majira ya saa tatu kwa baadhi wanafunzi kuwazuia wenzao
wasiingie katika chumba cha mtihani na baada ya hapo wakaibuka na
mabango kwenda katika ofisi za utawala wa chuo hicho.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo katika chuo hicho,Rais wa Serikali wa Chuo
Kikuu cha Kampala(Kiupeso),Elias Mbogho amesema kuwa maandamano hayo
yametokana na baadhi ya wanafunzi waliohitimu ngazi ya cheti ya ufamasia
kudai leseni na kuambiwa chuo hakitambuliki ndipo chanzo kiliazia hapo.
Mbogho
amesema kuwa hatua mbalimbali zilishapita na kujiridhisha kuwa
kinatambulika lakini wanafunzi wakitivo hicho wameendelea kuweka
malumbano.
Afisa
uhusiano wa chuo hicho ,Keneth Uki amesema kuwa mgogoro huo ulishapewa
suluhu kwa kupitia hatua za mamlaka za serikali na kudhibitisha
kutambuliwa chuo hicho.
Chapisha Maoni
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.