Waziri
wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu na balozi wa marekani Mark
Childress wakisaini mkataba wa dola Za kimarekani million 14.5 katika
hotel ya Treetops Lodge ilivyo hifadhi ya wanyamapori inayosimamiwa na
wananchi (WMA) ya Randlen monduli Arusha Kwa ajili ya mradi wa kulinda
mazingira, kukuza uhifadhi na utalii nchini Tanzania. (Picha na Loveness
Bernard)
Waziri wa maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu akibadilishana mkataba na balozi wa marekani Mark Childress.
Serikali iya Marekani imetoa zaidi ya dola Bilioni 30 kwa ajili ya Kulinda mazingira, Kukuza uhifadhi na Utalii nchini.
Hafla
ya kutiliana saini ilifanyika jana, Seronela mkoani Arusha ambapo
waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu na Balozi wa Marekani
nchini, Mark Childress walisaidni mmakubaliano ya dola 2milioni kwa
ajili ya kuendeleza mapambano ya ujangili n anyingine milioni 14.5 kwa
ajili ya uhifadhi.
Balozi
huyo wa Marekani Mark Childress, alimwelezea Nyalandu, kuwa ni
mwanasiasa jasiri na makini asiyeogopa kusema ukweli hata kama unaumiza.
Balozi
Childress amesema waziri huyo ni tofauti na wanasiasa wengine na
kwamba, ujasiri wake katika utendaji unapaswa kuungwa mkono. Kauli ya
Balozi huyo imetokana na uamuzi wa Nyalandu kuweka hadharani idadi ya
tembo waliopo nchini na kueleza bayana kuwa, tatizo hilo bado ni janga
kwa taifa.
“Kwa
mwanasiasa mwingine ingekuwa ngumu kutoa taarifa kama ile kwani angeona
anajimaliza lakini alilazimika kufanya hivyo ili njia za kutokomeza
tatizo hilo ipatikane na sasa marafiki wa uhifadhi tumeamua tupambane
pamoja kulaliza tatizo hili”.
Pia,
katika taarifa yake Nyalandu hakusita kueleza kutoweka kwa tembo 10,000
ambao hawakuweza kuonekana wakati wa sensa ya mwaka 2014 iliyofanywa na
Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori (TAWIRI) kwa kushirikiana na
mashirika ya kimataifa.
Akizungumza
wakati wa kutia saini makubaliano na uzinduzi wa mradi mkubwa wa
kulinda mazingira, kukuza uhifadhi na utalii nchini wa PROJECT, ambapo
serikali ya Marekani imetoa zaidi ya sh. Bilioni 31 katika utekelezaji
wa mradi huo.
Uzinduzi
huo ulifanyika jana katika hoteli ya Treetops iliyopo ndani ya eneo la
Hifadhi ya Wanyamapori inayosimamiwa na jamii (WMA) kwenye Hifadhi ya
Taifa ya Tarangire.
“Nyalandu
ni mwanasiasa na kiongozi jasiri, taarifa ya sensa ya tembo ilikuwa na
maeneo ambayo hayakuwa rahisi kuyasema, lakini aliamua kutangaza ili
dunia ifahamu tatizo la ujangili lililopo Tanzania.
“Hii
ni nadra sana kutokea kwa wanasiasa na ndio sababu Marekani imeamua
kutoa msaada wa haraka katika kusaidia vita dhidi ya ujangili kwenye
ushoroba wa Tarangire,” alisema Balozi Childress.
Aliongeza
kuwa msaada mwingine wa haraka utatolewa kwenye maeneo mengine ya
hifadhi ambayo kuna tatizo kubwa la ujangili ili kuhakikisha tembo
wanakuwa salama.
Kwa
upande wake, Nyalandu alisema serikali ya Rais Jakaya Kikwete,
imedhamiria na imejipanga kikamilifu kuhakikisha inashinda vita dhidi ya
ujangili na kwamba, itakuwa endelevu.
Alisema
tatizo la ujangili bado ni kubwa licha ya mafanikio makubwa kuanza
kuonekana kwa tembo kuanza kuongezeka kwenye baadhi ya hifadhi na mapori
ya akiba nchini.
Aidha,
alishukuru serikali ya Marekani kuendelea kuwa mshirika mkubwa wa
uhifadhi na kusaidia mapambano dhidi ya ujangili nchini na kwamba, wadau
zaidi hawana budi kuunga mkono jitihada hizo.
Pia,
alisema serikali itaendelea kuboresha maslahi na kutoa vitendea kazi
vya kutosha kwa askari wa wanyamapori nchini kwani, wamekuwa wakifanya
kazi kubwa ya kulinda maliasili za taifa.
Alisema
askari hao wamechagua kutoa maisha yao kwa uhifadhi na kulinda
wanyamapori hivyo, serikali inathamini mchango huo na itaendelea
kuwaboreshea maslahi na vitendea kazi.
Chapisha Maoni