Ni mwenyekiti wa tume ya taifa ya uchaguzi NEC Jaji Mstaafu Damiani
Lubuva akielezea masikitiko ya tume kufuatilia kile alichokiita ni
kuingiliwa kwa maafisa wa tume katika kazi zao za uandikishaji katika
miji ya Arusha na Kilimanjaro jambao lililopelekea kuzuka kwa vurugu
katika baadhi ya vituo ndani ya mikoa hiyo.
Jaji Damian amesema katika mahojiano yake maalum na ITV jijini Dar
es Salaam, kuwa tangu kaunza kwa zoezi la uandikishaji kumekuwa na
changamoto kadha ambazo hata hivyo tume ilijitahidi kuzitatua lakini kwa
hali ya Arusha na Kilimanjaro huenda tume ikalazimika kufanya maamuzi
magumu.
Amesisitiza kuwa ni vema viongozi wa kisiasa wakahakikisha wanakuwa
mstari wa mbele katika kufanikisha zoezi hilo ambalo kwasasa limekwisha
kukamilika kwa zaidi ya asilimia 85, ambapo pia amesisitiza kuwa kwa
hali ilivyo hivi sasa uchaguzi utafanyika kama ulivyopangwa kwani kila
kitu kiko katika hali ya ukamilifu.
Katika mahojaino hayo pia jaji Lubuva amezungumzia suala la
uandikishwaji kwa upande wa Zanzibar ambapo anasema zoezi hilo
linatarajia kuanza muda wowote akuanzia sasa huku akisisitiza utulivu
wakati wa zoezi hilo.
Chapisha Maoni