0
Matokeo ya uchaguzi wa ubunge Ethiopia

Chama tawala cha EPRDF chashinda uchaguzi wa ubunge nchini Ethiopia

Chama tawala cha Ethiopia EPRDF pamoja na washirika wake, kimeshinda viti 546 kati ya 547 bungeni kwenye uchaguzi uliofanyika tarehe 24 mwezi Mei mwaka huu.
Tume ya uchaguzi nchini Ethiopia NEBE, ilitangaza matokeo ya mwisho ya uchaguzi huo siku ya Jumatatu ambapo chama tawala kilitangazwa kushinda viti 500 vya bunge.
Viti vingine 46 vya bunge vilishindwa na wanasiasa wanaokiunga mkono chama tawala cha EPRDF ikiwa 24 ni kutoka chama cha SPDP, 9 kutoka chama cha BGPDP, 8 kutoka chama cha ANDP, 3 kutoka chama cha GPUDM, 1 kutoka chama cha HNL na kingine 1 kutoka chama cha APDO.
Kwa mujibu wa mwenyekiti wa NEBE Merga Bekana, kiti kimoja cha bunge kilichobakia bado hakijabainishwa mshindi wake.
Kulingana na takwimu za NEBE, asilimia 93.2 ya wananchi milioni 36.8 waliojisajili, ndio waliojitokeza kupiga kura siku ya uchaguzi.TRT SWAHILI

Chapisha Maoni

 
Top