WAMASAI KUOKOA JAMII YA VIFARU
Jamii ya wamasai Afrika mashariki ni jamii ambayo anatambulika kama jamii ya wawindaji mahiri.
Katika mila na tamaduni za kimasai, mtoto anapofikia umri wa kukatwa jando hutumwa kuwinda simba.
Kijana iwapo atafaulu kazi aliotomwa basi katika jamii atakuwa mtu mwenye kuheshimika na mwenye hadhi kubwa.
Unapokuwa katika mbuga ya Ol Pejeta, wanyama kama tembo, vifaru, simba na wanyama pori wengine huonekana wakiwa huru.
Wasai 11 ambao wanahusika na kulinda wanyama wanaotishiwa kamalizika wamefahamisha kuwa wameumua kuanza kucheza mchezo wa "cricket" wakiwa na nia ya kuwalinda vifaru wanaotishiwa kumalika.
Vifaru wanaotishiwa kumalizika kwa kuwindwa na wawindaji harumu ni vifaru wanaoitwa "vifaru weupe" ambao Kenya inawamiliki wakiwa idadi ndogo.
Richard Vigne, mkurugenzi katika mbuga ya Ol Pejeta Conservancy alifahamisha kuwa wamasai na utamaduni wao wa kuwinda sasa wamechukuwa uamuzi wa kuokoa wanyama.
Kutoka na tishio la kutoeka kwa vifaru hivyo, wanasayansi wanafanya utafiti ili kujaribu kuokoa jamii hiyo ya vifaru kwa utaalamu wa kisasa kama vile kupandikiza mbegu za uzazi.
Licha yakufanya utafiti, wanasayansi hao wamefahamisha kuwa mbegu za vifaru weupe wanopatikana nchini Sudani ni hafif una vigumu kudunga mimba kwa kifaru dike.
Utafiti unaendelea ili kuokoa jamii hiyo ya vifaru.TRT SWAHILI
Chapisha Maoni