Ujumbe wa Tanzania unaendelea kushiriki katika kikao cha Mkutano Mkuu
wa Kumi na saba wa Shirikia la Hali ya Hewa Duniani (WMO-Congress 17),
mijini Geneva, nchini Uswisi. Ujumbe huo umeshiriki katika matukio
mbalimbali ya mkutano huo ikiwa ni pamoja na Dkt. Agnes Kijazi kushiriki
katika siku ya Jinsia ya WMO (WMO Gender Day), kutoa mada zilizotoa
uzoefu wa Tanzania wa utekelezaji wa program za utekelezaji wa programu
ya utoaji wa huduma bora za hali ya hewa kwa jamii “Global Framework for
Climate Services (GFCS) na programu ya uendelezaji wa mitandao ya
upimaji wa hali ya hewa na mawasiliano (WMO Integrated Observation
System and WMO Information System-WIGOS/WIS). Kwa habari zaidi angalia
picha za matukio mbalimbali ya Mkutano huo hapa.
Mh. Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa
Mataifa, Geneva na Murugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Dkt. Agnes
Kijazi na Ujumbe wa Tanzania wakishiriki katika Mkutano Mkuu wa Kumi na
Saba wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO- Congress-17), Geneva,
Uswisi
“WMO Gender Day”, Siku ya Ijumaa, Tarehe 5 Juni 2015 ilikuwa siku ya
Jinsia (WMO Gender Day) ya Mkutano wa Kumi na saba wa Shirika la hali ya
hewa Duniani (WMO-Congress 17). Dkt. Agnes Kijazi, Mkurugenzi Mkuu wa
Mamlaka ya Hali ya Hewa na Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika
Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) alikuwa miongoni mwa zaidi ya
wajumbe 50 na wafanyakazi wa WMO walioshiriki katika ufunguzi wa siku
hii na kujadili masuala mbalimbali katika nyanja ya usawa na uwezeshaji
wa wanawake katika taasisi za hali ya hewa na WMO. Maoni yaliyotokana na
majadiliano ya siku hii yatajumuishwa na kutengeneza Mpango Mkakati wa
WMO utakaolenga masuala ya jinsia (WMO Gender Action Plan)
Vile vile siku ya tarehe 6 Juni 2015, Dr. Kijazi alishiriki katika
warsha ya Uongozi ya viongozi wanawake ikiwa na lengo kuwajengea uwezo
zaidi wa uongozi wajumbe waliohudhuria katika mkutano mkuu wa kumi na
saba wa WMO.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania, Dr Agnes Kijazi
akiwasilisha mada ya uzoefu wa Tanzania katika utoaji wa huduma za hali
ya hewa kwa jamii (Global Framework for Climate Services (GFCS)) katika
Mkutano Mkuu wa Kumi na Saba wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO
Congress-17), Geneva, Uswisi.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dr. Agnes
Kijazi akiwasilisha mada ya uzoefu wa Tanzania katika utekelezaji wa
Programu ya "WMO Intergrated Global Observation Systems (WIGOS)" katika
Mkutano Mkuu wa kumi na saba wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO),
Geneva, Uswisi.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dr. Agnes
Kijazi na Mkurugenzi wa utabiri Dr. Hamza Kabelwa wakiwa katika
majadiliano na maafisa wa Shirika la Hali ya hewa Duniani (WMO) na
Marekani wakati wa majadiliano yanayohusu namna ya kuboresha huduma za
hali ya hewa kwa jamii hususan utoaji wa tahadhari “ Early Warning”
katika Mkutano Mkuu wa kumi na saba wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani
(WMO), Geneva, Uswisi.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dr. Agnes
Kijazi na Mtabiri Mwandamizi katika Ofisi ya Mahusiano ya Kimataifa ya
TMA, Ndugu. Wilbert Timiza wakifuatili mwenendo wa Mkutano Mkuu wa kumi
na saba wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO), Geneva, nchini Uswisi.







Chapisha Maoni