Bendi maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya Ngoma Africa band aka
FFU-ughaibuni,yenye makao nchini Ujerumani,inatarijiwa kutumbuiza katika
maonyesho makubwa ya muziki na utamaduni Mamling Festival siku ya
jumapili alhasiri katika viwanja vya Schlosspark,Mamling 3, Mining
nchini Austria. watayarishaji wa onyesho hilo wameitaja bendi hiyo ya
Ngoma Africa band kuwa muziki wake ni sawa na mzimu unawapeleka puta
washabiki katika maonyesho ya kimataifa na washabiki nchini Austria
wanameisubiria kwa muda wa mwaka mzima. Kikosi kazi hiko chenye tabia ya
kuwatia kiwewe washabiki wake kila waendako na kujizolea washabiki
lukuki kote duniani,kinaupeleka muzimu wa Bongo Dansi nchini Austria
.Ziara ya bendi hiyo imeingiliana na mwezi wa Ramadhani wakati baadhi ya
wanamuziki wapo katika swaumu lakini
watatekeleza wajibu wao.
Ngoma Africa band iliyoanzishwa mwaka 1993 na kiongozi wake Ebrahim
Makunja almaarufu Kamanda Ras Makunja ni bendi iliyobatizwa majina mengi
ya kiusanii kutoka kwa washabiki majina kama FFU-Ughaibuni, "Watoto wa
Mbwa",Viumbe wa ajabu "Anunnaki Alien' na mengi mengineyo. ni bendi
yenye utajiri ya wanamuziki waliojaa vipaji, na kwa sasa inatamba na
nyimbo zake mbili
mpyakatika CD " La Mgambo" za kumuaga Rais Jakaya Kikwete anayemaliza muda .
Sikiliza at
wasiliana nao at ngoma4u@gmail.com
Chapisha Maoni