0


MSANII wa filamu za kibongo nchini, Shamsa Ford, amesema hajutii kuachana na mzazi mwenzake kutokana na matukio mabaya aliyokuwa akimfanyia akiwa ndani ya ndoa.

Akizungumza na gazeti la Staa Spoti, anasema hafikirii kama kuna mwanamke mvumilivu kama yeye kwa mwanaume huyo ambaye hata akimpa mwanamke yeyote mwezi mmoja akae naye hawezi kumaliza.

Anasema maisha yake ya ndoa yalikuwa mazuri kwa muonekano wa nje kwasababu alikuwa hawezi kuweka wazi mabaya ya aliyekuwa mume wake lakini alikuwa anaumizwa.





"Nilikuwa nampenda ndio maana nilikuwa namvumilia lakini siamini kama kuna mwanamke mwingine yeyote ambaye anaweza kumvumilia huyo mwanaume kutokana na tabia zake mbaya," alisema.

Shamsa alitumia nafasi hiyo, kuwaomba radhi rafiki wa aliyekuwa mume wake kutokana na kuwatukana kutokana na kuamini kuwa ndio waliokuwa wanamfundisha tabia mbaya kutokana na kuwa naye karibu.

Chapisha Maoni

 
Top