Deogratius Mongela na Chande Abdallah
KINDUMBWENDUMBWE! Mbunge wa Mbeya Mjini kwa ‘leseni’ ya Chama Cha
Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Joseph Osmund Mbilinyi ‘Sugu’
amemfikisha kortini aliyekuwa mkewe, Faiza Ally akitaka apewe mtoto
wao, Shaa (2) ili amlee kwa vile mama yake huyo si mwadilifu.
Aliyekuwa mkewe na mbunge wa mbeya mjini Joseph Osmund Mbilinyi ‘Sugu’, Faiza Ally akiwa katika pozi.
Ijumaa iliyopita, saa 2:00 asubuhi, Faiza alipanda kwenye kizimba cha
Mahakama ya Mwanzo, Manzese/ Sinza iliyopo Sinza-Makaburini jijini Dar
kwa ajili ya kukabiliana na madai hayo.
ZILIPO HASIRA ZA SUGU
Kwa mujibu wa chanzo chetu kilichomwaga ‘ubuyu’ huo, Mheshimiwa Sugu
alifikia hatua hiyo baada ya kuchukizwa na tabia mbaya za mwanamke huyo
hasa ya kuvaa nguo zinazomuacha nusu utupu na kupiga picha za aibu,
akiamini kuwa, tabia hizo zinaweza kuathiri makuzi ya mtoto huyo.
Mnyetishaji huyo aliendelea kusema kuwa, kwa kipindi kirefu, Sugu
amekuwa akimvumilia Faiza, lakini hivi karibuni uzalendo ulimshinda
baada ya picha zake akiwa amevaa kigauni kifupi na makalio nje kusambaa
mitandaoni.
PALIPOKOLEZEA HASIRA
Faiza alivaa kivazi hicho hivi karibuni kwenye hafla ya ugawaji wa Tuzo za Kili Music iliyofanyika Ukumbi wa Mlimani City, Dar.
SUGU MBELE YA HAKIMU
Akizungumza mbele ya hakimu mfawidhi wa mahakama hiyo, Patrick Vaginga,
Mheshimiwa Sugu alidai kuwa mbali na mzazi mwenzake huyo kuwa na tabia
ya kuvaa nusu utupu pia ana mtindo wa kupiga picha zisizo na maadili na
kuziweka mtandaoni yeye mwenyewe.
KUHUSU MTOTO
Sugu alikwenda mbele zaidi kwa kudai kwamba, pia mwanamke huyo amekuwa
na tabia ya kumpiga picha mbaya mtoto wao na kuzimimina humohumo
mitandaoni jambo ambalo alisema linamharibu mtoto huyo.
FAIZA HANA PESA
Mbali na sababu hizo, pia Sugu aliongeza kuwa, Faiza hana kipato kizuri
cha kuweza kumlea mtoto na mara kwa mara amekuwa akisafiri jambo ambalo
husababisha mtoto huyo kutopata malezi ya mama kwa muda mrefu hivyo
kuiomba mahakama impe haki yeye ya kuishi na mwanaye.
FAIZA AJIBU MAPIGO
Naye Faiza akijibu mapigo katika utetezi wake alisema kuwa, Sugu hafai
kumlea mtoto huyo kwa sababu naye ana tabia ya kusafiri kwa muda mrefu
hivyo kuishi mbali na mtoto ambapo aliiomba mahakama hiyo isimruhusu
baba mzazi huyo kuishi na mtoto kwa kuwa atamharibu.
KESI YAPIGWA KALENDA
Mheshimiwa Hakimu Vaginga akasema kwa vile kesi hiyo ndiyo imeanza
kusikilizwa kwa mara ya kwanza aliiahirisha hadi baadaye mwezi huu
ambapo hukumu itatolewa.
SUGU NJIA YAKE, FAIZA NJIA YAKE
Ijumaa Wikienda lililokuwa mahakamani hapo, liliwashuhudia wazazi hao, kila mmoja akiondoka na njia yake.
KWA NINI FAIZA NI MKE WA SUGU?
Kwa sheria za Kitanzania, mwanamke na mwanaume wakiishi pamoja kwa zaidi
ya miezi sita, hao tayari ni mke na mume kama ilivyokuwa kwa Faiza na
Sugu ambao waliishi pamoja kwa zaidi ya miaka miwili.
Chapisha Maoni