0
Vidal anusurika kifo kwenye ajali ya gari
Nyota wa Chile Arturo Vidal apata ajali alipokuwa akiendesha gari akiwa amelewa
Kiungo wa kati wa Juventus na timu ya taifa ya Chile Arturo Vidal, alinusurika kifo kwenye ajali ya gari iliyozuka katika mji mkuu wa Santiago.
Vidal mwenye umri wa miaka 27 alipata ajali hiyo akiwa na mkewe kwenye gari, kupata majeraha madogo. Baadaye Vidal alitiwa mbaroni na polisi baada ya kugunduliwa kuwa alikuwa amelewa. 
Hali ya afya ya Vidal inaarifiwa kuwa vizuri bila matatizo yoyote.
Hata hivyo, Vidal anasemekana kwamba atatimuliwa kutoka kwenye kikosi cha timu ya taifa yaChile na kufikishwa mahakamani kutokana na kosa la kuendesha gari akiwa amelewa.
Timu ya taifa ya Chile iliyokusanya pointi 4 katika mechi 2 zilizochezwa kwenye mashindano ya Copa America, huenda ikawa na wakati mgumu kwenye michuano hiyo kwa kukosa huduma yaVidal aliyeifungia mabao matatu.CHANZO TRT SWAHILI

Chapisha Maoni

 
Top