Watoto 250,000 wahofiwa kukabiliwa na baa la njaa Suda Kusini
UN imefahamisha kwamba watoto 250,000 wanakabiliwa na baa la njaa nchini Sudan Kusinikutokana na mapigano yanayoendelea tangu mwaka 2013.
Nchi ya Sudan Kusini ilijinyakulia uhuru mwaka 2011 lakini baadaye ikajikuta kwenye mizozobaada ya mapigano kuzuka Desemba mwaka 2013 kati ya wafuasi wa Rais Salva Kiir na wapinzani wanaoongozwa na aliyekuwa makamu wa rais Riek Machar.
Mizozo hiyo ilizidi kuongezeka miongoni mwa jamii ya Sudan Kusini na hatimaye kugeuka kuwa vita vya kikabila baina ya watu wa kabila la Dinka akiwemo Kiir kwa upande mmoja, na watu wa kabila la Nuer akiwemo Machar kwa upande mwingine.
Vita hivyo vya kikabila vilisababisha maelfu ya raia wa Sudan Kusini kupoteza maisha, huku raia wengine wapatao milioni 1.9 wakilazimika kuhama makazi yao.
Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na msimamizi wa masuala ya kibinadamu wa UN Toby Lanzer, mmoja kwa kila watoto watatu wanakumbwa na tatizo la utapiamlo huku watoto 250,000 wakikabiliwa na baa la njaa.
Chapisha Maoni