Danny Paul Njau, akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo.
Mshindi wa mchezo wa kubahatisha
wa Jay Millions, Danny Paul Njau (kushoto), akizungumza na waandishi wa
habari Dar es Salaam leo, kuhusu Kampuni ya Simu ya Vodacom kushindwa
kumpa zawadi yake ya sh.milioni 100 baada ya kushinda mchezo huo.
Mshindi wa mchezo wa kubahatisha wa Jay Millions, Danny Paul Njau
(kulia), akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu
Kampuni ya Simu ya Vodacom kushindwa kumpa zawadi yake ya sh.milioni 100
baada ya kushinda mchezo huo. Kushoto ni mtoto wake, Erick Danny Njau.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Na Dotto Mwaibale
MSHINDI wa mchezo wa kubahatisha wa Vodacom Jay Millions Danny Paul Njau
kupitia jina la Innocent Daniel Njau ametishia kwenda Mahakama
kuishitaki kampuni ya simu ya Vodacom kwa kushindwa kumpa zawadi yake ya
ushindi sh.milioni 100 baada ya kushinda mchezo wa kubahatisha wa
Vodacom Jay Millions.
Njau ametoa siku saba kwa kampuni hiyo kuhakikisha inampatia fedha hizo vinginevyo atakwenda mahakama kutafuta haki yake.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi Njau
alisema amesikitishwa na danadana anazopigwa na kmapuni hiyo kushindwa
kumpatia kitita chake hicho baada ya kushinda.
"Tayari nimetoa malalamiko yangu kwa Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Michezo
ya Kubahatisha kuhusu suala hilo lakini mpaka hivi sasa bado
hajafanikiwa" alisema Njau.
Njau alisema kwamba tangu kampuni hiyo ianze kucheza mchezo huo alikuwa
akishiriki kucheza kila siku na ilipofika Januari 14, 2015 saa 5:8
asubuhi kupitia simu yake alipokea ujumbe sms iliyosomeka hivi 'hongera
wewe ni mshindi wa leo wa Tzs Miliioni 100 utapigiwa simu na wafanyakazi
wa Vodacom. Kwa maelezo zaidi ndani ya masaa 48 ambapo alisubiri bila
ya kupigiwa simu kama alivyoelekezwa.
Alisema Januari 20, 2015 alienda ofisi za vodacom na kuwaelezea kuhusu
jambo hilo ambapo aliambiwa awape muda na aliporudi Januari 22
alikutanishwa na maofisa wa Jay Millions na kufanyanao kikao akiwepo
mwakilishi kutoka bodi ya michezo ya kubahatisha ambapo aliambiwa kuwa
eti sms hiyo ni ya kwao lakini ilitoka mapema kwenda kwake.
Njau alisema kwamba kauli hiyo ilimshangaza sana ukizingatia kuwa katika
kipindi hicho cha mchezo kulikuwa na matangazo yaliyokuwa yakisema kila
siku kutakuwa na mshindi mmoja wa sh.100, washindi 10 milioni 10 na
washindi 100 wa sh.milioni 1 na kuwa yeye alifuata taratibu zote za
kucheza mchezo huo Jay kwenda 15544 na kuona sms ya ushindi.
Alisema baada ya majadiliano na maofisa hao walimuuliza wampe sh. ngapi
kwa kuwa zawadi hiyo imetoka mapema na kabla ya watu hawacheza na kuwa
wao hawana pesa nyingi anayoifikiria.
Alisema hakuamini kilichokuwa kikifanywa na kampuni hiyo katika
uchezeshaji wa mchezo huo na kuwa aliomba apewe muda wa kutafakari
ambapo aliamua kupeleka malalamiko yake kwenye bodi ya michezo ya
kubahatisha na kwenye vyombo vya habari.
Jitihada za mtandao huu kumpata mmoja wa maofisa wa Vodacom Tanzania
ambaye alitajwa kuwa ni Meneja, Kelvin Twisa ili kutoa ufafanuzi wa
madai hayo zilishindikana baada ya simu yake ya mkononi kupigwa zaidi ya
mara nne bila ya kupokelewa, pia hali kama hiyo ilitokea kwa Mkurugenzi
Mkuu wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, Tarimba Abbas Tarimba ambaye
simu yake ilikuwa imefungwa jitihada hizo zinaendelea ilikutoa fursa kwa
maofisa hao kutoa ufafanuzi ili umma wa watanzania upate kujua
kinachoendelea katika kampuni hiyo.
(Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com)
Chapisha Maoni
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.