WATU 64 WAFARIKI KWA JOTO PAKISTAN
Baadhi ya watu 15 wamefariki kufatia joto kali katika mji wa Karachi ambapo kiasi cha joto kufikia nyuzi joto 41.
Watu wengine 10 wamefariki katika mji wa Sibbi, Tharparkar na Shekhupur siku ya Jumamosi.
Daktari Seemi Jamali wa hospitali ya Jinnah aliiambia shirika la habari la Anadolu "wagonjwa 30 waliletwa hosptali wakiwa na hali mbaya na wengine 15 wamefariki dunia ikiwa wengıne 15 wameanza matibabu katika mji wa Karachi."
Taarifa zinafahamisha kuwa zaidi ya watu 140 wamekwishafariki kutokana na joto hilo kali.
İdara ya hali ya hewa imetabiri kuendelea kwa joto kali kwa muda wa siku chache zijazo katika maeneo mengi ya nchi.
Hali hii itapelekea kukatika kwa umeme na kufanya mwezi wa Ramadhani kuwa mgumu.
Chapisha Maoni