0
Wanamgambo wa Taliban kushambulia bunge la Afghanistan

Wanamgambo wa Taliban kushambulia bunge la Afghanistan

Wanamgambo wa Taliban wameshambulia bunge la Afghanistan wakati wa kikao jumatatu.
Fatullah Qaisari, Mbunge kutoka mji wa Faryab, aliliambia shirika la habari la Anadolu kuwa milipuko ilisikika nje ya jengo ila wanamgambo hawakuweza kuingia katika jengo la Bunge.
Qataira alisema kuwa wanamgambo hao walirusha mabomu wakiwa wamejificha katika majengo pembezuni mwa jengo la Bunge.
Aliendelea kufahamisha kuwa spika wa bunge alipelekwa katika jengo lenye usalama na wengine kadhaa wameripotiwa kujeruhiwa.
Taliban wamedai kwamba baadhi ya washambuliaji wametokea bungeni huku Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani Sediq Sediqqi amesema kuwa vikosi maalum vimesambazwa kila mahali ili kuleta usalama ndani ya nchi. TRT SWAHILI

Chapisha Maoni

 
Top