0
Neymar atupwa nje ya Copa America

Shirikisho la mpira la Amerika ya kusini limetoa hukumu ya kumfungia Neymar mechi 4

Hukumu iliyotolewa ya kumfungia mechi nne nyota wa Barcelona na nahodha wa timu ya taifa ya Brazil, Neymar Jr imemsababishia nyota huyo kutoshiriki mchezo wowote uliosalia katika Copa America.
Neymar alipata adhabu hiyo baada ya kumpiga na mpira mchezaji wa Colombia ambapo katika mechi hiyo Brazil ililala kwa goli moja kwa nunge.
Brazil ilitinga uwanjani Jumapili kukipiga na Venezuela na kuweza kuibuka na ushindi wa magoli 2 kwa moja.
Nyota wa Barcelona na mshindi mara nne wa tuzo ya Ballon d’Or, Lionel Messi alielezea kusikitishwa kwake na hukumu hiyo iliyompata Neymar.
Messi alisema kuwa Neymar ni mchezaji muhim kwa Brazil na Brazil imepata pengo.

Chapisha Maoni

 
Top