0
Balozi mpya wa Misri nchini Israel ataeuliwa

Misri yamteua balozi wake mpya nchini Israel kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2012

Rais Abdel Fattah al-Sisi, amemteua Hazem Khairat kuwa balozi mpya wa Misri nchini Israel siku ya Jumapili kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2012.
Sisi amemteuwa Hazem Khairat ili kuchukuwa nafasi ya balozi wa zamani Atef Salem, aliyekuwa akihudumu katika ubalozi wa Misri ulioko mjini Tel Aviv nchini Israel.
Wakati huo huo, Atef Salem anaarifiwa kuteuliwa kuwa balozi mpya wa Misri nchini Cuba.
Israel ilimkaribishwa balozi mpya wa Misri siku ya Jumapili baada ya miaka mitatu ambapo serikali ya Misri ilichukuwa hatua ya kufunga ubalozi wake kufuatia maandamano ya ghasia kati ya Israel na Hamas katika ukanda wa Gaza.
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu alisema kwamba ubalozi huo utasaidia kuboresha uhusiano na kuimarisha amani kati ya nchi zote mbili. TRT SWAHILI

Chapisha Maoni

 
Top