0
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Rajab Luhwavi akimkaribisha  Mgombea Urais wa chama cha Mapinduzi CCM Dk.John Pombe Magufuli  awasalimie wananchi,awashukuru na kujitambulisha kwa wananchi hao waliokuwa wamekusanyika kwa wingi nje ya ofisi za CCM Manyoni mkoa wa Singida.
  Mgombea Urais wa chama cha Mapinduzi CCM Dk.John Pombe Magufuli  akiwasalimia wananchi waliokuwa wamekusanyika kwa wingi nje ya ofisi za CCM Manyoni mkoa wa Singida. 
  Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk.John Pombe Magufuli(kulia) akisalimiana na aliyekuwa Mbunge wa Nzega Vijijini Dk. Hamisi Kigwangala
 Hussein Bashe ambaye ametia nia ya kugombea ubunge jimbo la Nzega Mjini akisalimiana na Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk.John Pombe Magufuli mjini Nzega. 
 Wananchi wa Nzega wakishangilia mara baada ya kumisikiliza  Mgombea Urais wa chama cha Mapinduzi CCM Dk.John Pombe Magufuli  alipomaliza kuwasalimia na kuwashukuru kwa namna walivyojitokeza kumtia moyo,nje ya  za CCM Nzega
 Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk.John Pombe Magufuli akiwasalimu wakazi wa Nzega kwenye mkutano uliofanyika nje ya ofisi ya CCM wilayani hapo, ambapo aliwaambia Wananchi kuwa amefarijika na mapokezi mazuri na amewaahidi kurudi tena wakati wa kampeni zitakapoanza..
  Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk.John Pombe Magufuli akisaini vitabu vya  wageni Ofisi za CCM ndani ya mji wa Manyoni  mkoani Singida alipokuwa akipita kuwashukuru Wananchi kwa kujitokeza kwa wingi kumpokea na kujitambulisha kwao akiwa anatokea jimboni kwake Chato akirejea jijini Dar kwa njia ya barabara.
 Wananchi wa Igunga wakiwa na Bango lao wakimkaribisha Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk.John Pombe Magufuli alipokuwa akiwasili maeneno hayo kuwashukuru na kujitambulisha kwao akiwa anatokea jimboni kwake Chato akirejea jijini Dar kwa njia ya barabara.

Wananchi wa Ikungi wakiwa wamelizunguka gari la Mgombea Urais wa chama cha Mapinduzi CCM Dk.John Pombe Magufuli na kufunga barabara wakimtaka awasalimie tu ndipo aendelee na safari yake.
 Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk.John Pombe Magufuli akiondoka nzega huku shangwe zikiwa zimetawala kutoka kwa mashabiki mara baada ya kuwashukuru kwa kujitokeza kwa wingi kumpokea na kujitambulisha kwao akiwa anatokea jimboni kwake Chato akirejea jijini Dar kwa njia ya barabara
 Wananchi wa Igunga wakimshangila  Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk.John Pombe Magufuli mara baada ya kuwashukuru kwa kujitokeza kwa wingi kumpokea,na pia alijitambulisha kwao.Dkt Magufuli aliwaeleza wananchi hao kuwa ana mambo ya kuwaambia lakini kwa sasa anapita kujitambulisha kwao,kwa sababu wakati wa kampeni bado haujafika,lakini ukifika basi atarejea tena kuzungumna nao kinagaubaga. 
 Wananchi wa Ikungi wakishangilia kwa ujio wa Mgombea Urais wa chama cha Mapinduzi CCM Dk.John Pombe Magufuli na kufunga barabara wakimtaka awasalimie tu ndipo aendelee na safari yake.
 Mgombea Urais wa chama cha Mapinduzi CCM Dk.John Pombe Magufuli  akiwasalimia wananchi waliokuwa wamekusanyika kwa wingi nje ya ofisi za CCM mkoa wa Singida.
  Mgombea Urais wa chama cha Mapinduzi CCM Dk.John Pombe Magufuli  akiwasalimia wananchi waliokuwa wamekusanyika kwa wingi nje ya ofisi za CCM mkoa wa Singida. 
Wananchi wa Singida na vitongoji vyake wakiwa wamekusanyika nje ya ofisi za CCM mkoa wa Singida,wakitaka kumuona na kumpongeza  Mgombea Urais wa chama cha Mapinduzi CCM Dk.John Pombe Magufuli kwa kuchaguliwa kuwa mgombea Uraisi wa CCM na pia kumuombea na kumtakia kila lakheri katika safari yake hiyo ya kugombea nafasi ya Uraisi
  Mgombea Urais wa chama cha Mapinduzi CCM Dk.John Pombe Magufuli  akiwashukuru Wananchi wa Singida mjini kwa kujitokeza kwa wingi kumlaki,walipokuwa wamekusanyika kwa wingi nje ya ofisi za CCM mkoani humo.
 Mh Mwigulu Nchemba akishangilia jambo mara baada ya kumsikiliza  Mgombea Urais wa chama cha Mapinduzi CCM Dk.John Pombe Magufuli alipokuwa akiwasalimia wananchi waliokuwa wamekusanyika kwa wingi nje ya ofisi za CCM mkoa wa Singida.
 Mgombea Urais wa chama cha Mapinduzi CCM Dk.John Pombe Magufuli  akisalimiana na mmoja wa makada wa CCM nje ya ofisi za CCM njini Manyoni Mkoani Singida,mara baada kuwasalimia,kuwashukuru Wananchi waliojitokeza kumpokea na pia alipata nafasi ya kujitambulisha kwa wananchi hao.

Chapisha Maoni

 
Top