Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa, Balozi Irene Kasyanju akitoa hotuba wakati wa kumuaga Balozi
wa Ubelgiji ambaye amemaliza muda wake wa kazi hapa nchini, Mhe. Adam
Koeler huku Balozi huyo (wa kwanza kulia waliketi) na wageni waalikwa
wakimsikiliza. Hafla hiyo ilifanyika katika Hoteli ya Serena Jijini Dar
es Salaam tarehe 22 Julai, 2015. Katika hotuba yake Balozi Kasyanju
alimsifu Balozi Koeler kwa kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na
Ubelgiji.
Balozi Koeler pamoja na Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika
katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Joseph
Sokoine wakimskiliza Balozi Kasyanju wakati wa hafla fupi ya kumuaga
Balozi Koeler.
Balozi Koeler nae akizungumza wakati wa hafla ya kumuaga. Katika
hotuba yake Balozi huyo aliishukuru Serikali ya Tanzania kwa
ushirikiano alioupata katika kipindi chote alichokuwepo hapa nchini na
kusifu ukarimu wa Watanzania.
Balozi Kasyanju kwa pamoja na Mkuu wa Mabalozi wanaowakilisha nchi
zao hapa nchini ambaye pia ni Balozi wa Congo (DRC), Mhe. Juma Halfan
Mpango na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, Bw.
Alvaro Rodrigues wakimsikiliza Balozi Koeler (hayupo pichani)
akihutubia.
Balozi Sokoine nae akizungumza machache wakati wa hafla ya kumuaga Balozi Koeler
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa, Bi. Zuhura Bunndala (katikati) akiwa na wageni
waalikwa wengine wakati wa hafla ya kumuaga Balozi wa Ubelgiji ambaye
amemaliza muda wake wa kazi hapa nchini
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali, Bi. Mindi Kasiga
(katikati) akiwa na Balozi wa Ujerumani hapa nchini, Mhe. Egon Kochanke
(kushoto) pamoja na Afisa Mambo ya Nje, Bi. Felister Rugambwa wakati wa
hafla ya kumuaga Balozi wa Ubelgiji.
Balozi wa Ireland hapa nchini, Mhe. Fionnuala Gilsenan (kulia) akiwa
na Bw. Rodrigues (kushoto) na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano
wa Kimataifa, Bi. Maulidah Hassan wakati wa hafla ya kumuaga Balozi wa
Ubelgiji
Wageni waalikwa wakati wa hafla hiyo
Bi. Kasiga ambaye alikuwa msheheshaji (MC) katika hafla hiyo akiwakaribisha Mabalozi na wageni waalikwa kwenye hafla hiyo
Kaimu Katibu Mkuu, Balozi Kasyanju (kushoto) na Balozi Koeler (kulia)
pamoja na wageni waalikwa wakimsikiliza Bi. Kasiga ambaye haonekani
pichani
Juu na Chini ni Maafisa Mambo ya Nje wakifuatilia matukio kwenye hafla ya kumuaga Balozi wa Ubelgiji.
Chapisha Maoni